Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Ofisi za CHADEMA zimechomwa moto" Makene Mkuu wa Mawasiliano CDM

OFISI WEB 660x400 "Ofisi za CHADEMA zimechomwa moto" Makene Mkuu wa Mawasiliano CDM

Fri, 14 Aug 2020 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa CHADEMA Tumaini Makene amesema kuwa tukio la ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini kuchomwa moto na wasiojulikana si jambo jema ukizingatia leo Mgombea Urais wa chama hicho Tundu Lissu atakuwa Arusha.

“Taarifa za awali usiku wa kuamkia leo watu wasiojulikana wamevamia na kumwagia Petroli jengo la Ofisi za Kanda ya Kaskazini, bahati mbaya hata mlinzi wa ofisi hizo hajulikani yuko wapi baada ya tukio hilo, ni tukio baya kwa sababu hata mgombea wetu wa Urais anaingia Jiji la Arusha leo” Makene

Ofisi za chama hicho Kanda ya Kaskazini zimeungua moto usiku wa kuamkia leo, baada ya watu wasiojulikana kumwagia Petroli jengo hilo na kisha kulilipua.

LIVE: RAIS MAGUFULI ANAZUNGUMZA NA BARAZA KUU LA KANISA LA TAG

Chanzo: millardayo.com