Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisi ya Msajili yaangushiwa jumba bovu migogoro ya kisiasa

Wazichapaa Data Ofisi ya Msajili yaangushiwa jumba bovu migogoro ya kisiasa

Wed, 25 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya viongozi wa vyama vya NCCR-Mageuzi na Chadema kumtupia lawama Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuchochea migogoro ndani ya vyama hivyo, kiongozi huyo amesema ofisi yake haichochea bali migogoro hiyo inaanzia ndani ya vyama vyenyewe.

Jaji Mutungi ametoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza na Mwananchi, juu ya tuhuma za kuhusika kuchochea mgogoro ndani ya chama cha NCCR Mageuzi ambao umepamba moto huku upande mmoja ukiituhumu ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuchochea mgogoro huo kwa kutambua upande ulioitisha mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho. “NCCR Mageuzi walikuwa na mkutano wao, wametualika wenyewe, tumetuma watu wa Ofisi ya Msajili, ameenda ndugu Nyahoza, bahati nzuri yanayotokea baada ya hapo ni Msajili, jamani Msajili hana nguvu kubwa sana ya kuingilia wanachama na kuunda kambi ndani ya vyama” alisema

Mei 21, Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi ilimsimamisha Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na Makamu Mwenyekiti (Bara), Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi Mkutano mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo, Mbatia na wafuasi wake wamepinga uamuzi huo wa Baraza Kuu wakisema ulikuwa ni mkutano batili na wanashangaa kuona Ofisi ya Msajili ikishiriki kwenye mkutano huo huku ikifahamu kwamba haukuwa halali.

Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la chama hicho, Mohamed Tibanyendela juzi alisema baada ya kikao cha Kamati Kuu kilichoitishwa na Mbatia, kwamba, hawatambui mkutano wa halmashauri kuu uliofanyika Mei 21 kwa sababu haukuwepo kwa mujibu wa Katiba.

Tibanyendela alisema Kamati Kuu ililaani Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuingilia migogoro ya vyama vya siasa na tayari wameshamwandikia Msajili wa Vyama vya Siasa barua na mamlaka yake ya uteuzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live