Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyalandu atangaza kutumia mbinu za CCM kuipa ushindi Chadema

91612 Pic+nyalandu Nyalandu atangaza kutumia mbinu za CCM kuipa ushindi Chadema

Mon, 13 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) kanda ya kati nchini Tanzania wametaja mikakati yao ikiwamo kishinda ubunge wa Dodoma Mjini.

Mwenyekiti wa chama hicho kanda ya kati, Lazaro Nyalandu ametoa kauli hiyo leo Jumapili Januari 12, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kanda za chama hicho jijini Dodoma.

Nyalandu amesema pamoja na kanda yake kuwa na majimbo 29, lakini anaangalia zaidi mahali ambapo kuna makao ya viongozi wa serikali na akasema ndiyo utamaduni kwa chama chao.

"Kama ni mbinu za ushindi nazijua kutoka  CCM hivyo nitatumia mbinu hizo kuwashinda na nitakuwa na zingine za kwangu lazima nibebe majimbo mengi, kikubwa naitaka Dodoma," amesema Nyalandu.

Mbunge huyo wa zamani wa Singida Kaskazini (CCM) ametaja sababu kubwa za kumpa tumaini la ushindi ni kuwa ana wanachama wengi kuliko chama kingine kwa takwimu walizofanya lakini akasema watumishi wengi wa serikali waliohamia Dodoma ni wanachama wao.

Katika hatua nyingine, Nyalandu amesema Chadema  kanda ya kati wameanza maandalizi ya kujenga ofisi yao jijini Dodoma ambayo itakuwa kubwa na nzuri ya mfano.

Pia, Nyalandu aliyewahi kuwa waziri wa maliasili na utalii amewataka wakulima kuzitumia mvua zinazonyesha kulima kwa bidii ili waweze kujitegemea kwa chakula na kuepuka kukaa vijiweni bila kufanya kazi.

Chanzo: mwananchi.co.tz