Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyalandu ajiapiza kutohama Chadema

44853 Pic+nyalandu Nyalandu ajiapiza kutohama Chadema

Tue, 5 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kurudi CCM akitokea Chadema, Mbunge wa zamani wa Singida Kaskazini ambaye kwa sasa ni kada wa Chadema, Lazaro Nyalandu amesema hakuletwa kwenye chama hicho na mafuriko.

Lowassa aliyerejea CCM wiki iliyopita alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 na kupitishwa kugombea urais kupitia chama hicho akiwakilisha pia vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwa na kundi kubwa la wana CCM waliohama naye wakifahamika kama mafuriko.

Hata hivyo, Nyalandu aliyejitoa CCM Oktoba 30, 2017 na baadaye kujiunga na Chadema jana alitumia akaunti yake ya Twitter kuandika ujumbe unaoelezea  hatima yake ndani ya Chadema.

“Naamini katika kushiriki kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania kupitia upinzani. Tusikate tamaa. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Nyalandu katika ujumbe huo.

Ujumbe huo umechagiwa na watu mbalimbali na miongoni mwao ni mark zack aliyesema, “Lowasa alisema ivo ivo. Ngoja tuone wakikunyima nafasi ya kugombea uraisi 2020 na 2025 tuone kama hujarudi kwa nzi wa kijani uko mnapopaita nyumbani.”

Naye Bura Bura amesema, “Kweli mze tena uliuacha na ubunge na maslahi yake kwa kuenda upande wa kuwa huru kutetea haki ,tupo pamoja mheshimiwa.”



Chanzo: mwananchi.co.tz