Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nsomba atetea uenyekiti CCM Mbeya Mjini

Mbeyaa Pic Data Nsomba atetea uenyekiti CCM Mbeya Mjini

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: Mwananchi

Afrey Nsomba ameweza kutetea kiti cha mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini baada kupata kura 873 na kuwabwaga wapinzani wake.

Nsomba amembwaga, Moses Mwisete aliyepata kura 186 huku Tumpale Laizer akipata kura tano katika uchaguzi uliofanyika jana Jumamosi Oktoba Mosi.

Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya Mjini, Denis Luhende amesema uchaguzi huo haukuwa na kashikashi kubwa kama miaka ya nyuma kutokana na wajumbe kuelewa na kutambua haki zao.

"Siku zote fujo zinatokana na msukumo wa wajumbe kumlazimisha mgombea agome au aanzishe fujo, lakini safari hii kila kitu kimekwenda sawa na wagombea wote wamekubali matokeo," alisema Luhende.

Wilaya nyingine uchaguzi wao unafanyika leo Jumapili Oktoba 2, 2022. Wilaya ya Mbeya Vijijini aliyeteuliwa ni Akimu Mwalupindi, Japhet Mwanasenga, Ramadhani Mwandala. Wilaya ya Rungwe yupo, Meckson Mwakipunga, Sam Mwakapala, Dk Salatie Mwakyambiki na Elizabeth Mwasonya.

Kwa upande wa Wilaya ya Chunya Noel Chiwanga na Shilla Sheyo wakati Mbalali yupo, Mbwilo Mary, Mgao Iganas, Kitalima Leonard na wilayani Kyela watakaotoana jasho kwenye kinyang'anyiro hicho ni Elias Mwanjala, Rahabu Kajenga pamoja na Patrick Mwampeta.

Chanzo: Mwananchi