Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nondo kuburuzwa mahakamani leo

Nondo 3243 Nondo kuburuzwa mahakamani leo

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo Abdul Nondo na wenzake wanne huenda wakafikishwa mahakamani leo tarehe 25 Machi kwa tuhuma za kufanya vurugu kwenye uchaguzi wa marudio wa Kata ya Kasingirima baada kumkamata kijana mfuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliyemuona na kura 'feki'.

Mbali na Nondo, viongozi na wanachama wengine wa Kigoma Mjini ambao wanatarajia kuburuzwa mahakamani ni pamoja na Mgombea udiwani kata ya Kasingirima, Alumbula Khalidi; Alhaji Mzee Selemani Simba, Ntakije Ntanena na Khamis Mzungu.

Makada hao wa ACT wazalendo walikamatwa na polisi siku ya uchaguzi katika kata ya Kasingirima- Kigoma Mjini tarehe 20 Machi 2024 baada ya kumzuia kijana wa anayedaiwa kuwa mfuasi wa CCM akiwa na kura bandia.

Akizungumza M, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Abdul Nondo amesema wamefunguliwa kesi na muda wowote kuanzia sasa wanaweza kupelekwa Mahakamani wakituhumiwa kufanya fujo katika kituo cha kupigia kura cha Mtaa wa Livingston -Kasingirima.

Amesema pia wanatuhumiwa kumshambulia kijana wa CCM, tuhuma ambazo amedai kuwa sio za kweli.

“Tumetakiwa wote kurejea Central Police Kigoma siku ya Jumatatu tarehe 25 Machi 2024. Nimewasilisha malalamiko yangu kwa OCD Kigoma Mjini na kufungua jalada la kesi kwa OCCID dhidi ya Polisi kituo kikuu aliyetumia"Unreasonable Force"dhidi yangu kwa kunipiga kinyume na PGO No. 15 na 16 tarehe 20/03/2024.

“Ni katika uchaguzi wa Kasingirima baada ya kutaka kijana aliyekuwa na kura bandia akamatwe. Nitafuata taratibu zote hadi hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya Askari huyu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live