Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nitaunda Serikali ya umoja wa kitaifa- Prof Lipumba

6bc003416d898f86e0414321d7415022 Nitaunda Serikali ya umoja wa kitaifa- Prof Lipumba

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kinataka nchi iwe na taasisi imara inayounda mfumo madhubuti usiojali chama gani kiko kwenye madaraka.

Akizungumza kwenye Kampeni mapema leo Magu, Mwanza, Mgombea urais wa Chama Cha Wananchi (CUF) imesema ikipewa dhamana itaunda mfumo unaohitaji nguvu ya pamoja na ushirikishwaji wa kila Mtanzania na kwamba kwa sababu hiyo CUF inapendekeza serikali ya umoja wa kitaifa.

“Serikali ya Umoja wa Kitaifa chini ya CUF itaweka misingi ya kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na Demokrasia ya kweli. Serikali ya umoja wa kitaifa itakamilisha mchakato wa kupata katiba mpya yenye misingi imara ya demokrasia na utawala bora.

“Katiba ambayo pamoja na mambo mengine itatenganisha kikamilifu mamlaka na nguvu za mihimili mbalimbali, italinda misingi ya ushindani wa kisiasa, itapanua na kukuza haki za kiraia, na itahakikisha uwepo wa uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari na fursa ya kujieleza,” alieleza Lipumba.

Chanzo: habarileo.co.tz