Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni vicheko tupu Mdee na wenzake walipokutana na Lema

Mdee Wenzake Lema.png Ni vicheko tupu Mdee na wenzake walipokutana na Lema

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Wabunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee na Ester Bulaya wamefurahia kukutana na mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa mara ya kwanza tangu aliporudi nchini akitokea Canada alikokimbilia baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Watatu hao walikutana jana Jumapili Aprili 23, 2023 katika Usharika wa Kondeni Matala mkoani Kilimanjaro kwenye ibada ya shukrani ya Mchungaji Eliona Kimaro iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT, Askofu Fredrick Shoo.

“Jana nilifarijika sana kuonana na Brother (kaka) Godbless Lema katika kazi ya Mungu! Katika nyumba ya Mungu, upendo miongoni mwetu haukujificha. Duniani tunapita tu. Hongera bro kwa kazi ya jana,” aliandika Mdee kwenye mitandao yake ya kijamii.

Naye Bulaya aliandika, “Ilikuwa siku ya furaha kukutana na kaka yetu Godbless Lema…Upendo ulitawala.’’

Chanzo: mwanachidigital