Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni mwendo wa kalenda tu kesi ya kina Mdee, Chadema

Mdeepiic Data Ni mwendo wa kalenda tu kesi ya kina Mdee, Chadema

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi ya wabunge 18 wa viti maalum waliovuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 imekwama kuanza kusikilizwa kutokana na kutokuwepo kwa mawakili wa Serikali, na hivyo imeahirishwa hadi Ijumaa ijayo, Oktoba 7, 2022.

Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama,kwa kwa utaratibu wa Mapitio ya Mahakama (Judicial Review).

Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, ilikuwa imepangwa kuanza kusikilizwa na Jaji Cyprian Mkeha, jana Ijumaa Septemba 30.2022.

Hata hivyo, mahakama imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo kutokana na jopo la mawakili wa Serikali, Stanley Kalokola, Boaz Msoffe na Leonia Maneno wanaomwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye ni mmoja wa wadaiwa kutokuwapo mahakamani.

Jaji Mkeha amesema Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (inayomwakilisha AG), ilimwandikia barua Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ikimjulisha kuwa jopo la mawakili wa Serikali wanaosimamia kesi hiyo hawatakuwepo leo na ikaomba isogezwe mbele hadi Oktoba 7.

Barua hiyo ya Septemba 21, 2022, iliyosainiwa na Lukelo Samuel kwa niaba ya Wakili Mkuu wa Serikali, ambayo Mwananchi limeiona nakala yake, inaeleza kuwa mawakili hao watakuwa wanahudhuria mkutano mkuu wa mwaka Mawakili wa Serikali.

Advertisement Kwa mujibu wa barua hiyo, mkutano huo ulioandaliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali unafanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 27-30 (leo).

“Tunaomba kwamba shauri hili liahirishwe na lipangiwe tarehe nyingine ya kusikilizwa”, inasomeka sehemu ya barua hiyo na kuopendekezwa lipangwe Oktoba 7 mwaka huu na kwamba wanaona kwmaba itafaa kulingana na ratiba ya mahakama na kuongeza:

Mawakili wa kina Mdee na wa Chadema hawakuwa na pingamizi na waliieleza mahakama kuwa nao walipata nakala hiyo ya barua ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndipo Jaji Mkeha akaahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 7, 2022.

Wadai katika kesi hiyo ni Chadema kupitia Bodi yake ya  Wadhamini na AG, ambaye pia anasimama niaba ya Bunge la Tanzania; na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Katika shauri hilo namba 36 la mwaka 2022, Mdee na wenzakeo wanaowakilishwa na mawakili  Panya, Aliko Mwamanenge, Edson Kilatu na Emmanuel Ukashu wanapinga uamuzi  uliotolewa na Baraza Kuu la Chadema wa Mei 11, 2022.

Wanaiomba mahakama hiyo ipitie mchakato na uamuzi huo wa Chadema kuwafukuza kisha itoe amri tatu.

Amri hizo ni ya kutengua mchakato na uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama (certiorari order), kukilazimisha Chadema kutimiza wajibu wake kisheria (mandamus), yaani kuwapa haki ya kusikiliza na amri ya zuio dhidi ya Spika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kutokuchukua hatua yoyote mpaka malalamiko yao yatakapoamuriwa.

Uamuzi huo wa Baraza Kuu ulitokana na rufaa walizozikata kina Mdee kupinga uamuzi wa awali wa kuwavua uanachama uliotolewa na Kamati Kuu, Novemba 27, 2020, iliyowatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, bila ridhaa ya chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live