Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni Dkt. Tulia, Spika Bunge la Tanzania!

Tuliapicc Data Dk. Tulia Ackson Spika Tanzania

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamempitisha Dkt. Tulia Ackson kuwa Spika wa Bunge hilo atakayeongoza hadi mwaka 2025 akichukua nafasi ya Job Ndugai aliyejiuzulu Januari 06, 2022.

Mwenyekiti wa Mkutano huo William Lukuvi, amemtangaza Dkt. Tulia kuwa Spika wa Bunge leo Februari 01, 2022 ambaye amepata jumla ya kura 376 kati ya 376.

Mchakato wa kumpata Spika umefanyika katika kikao cha kwanza cha Bunge ambapo wagombea wote tisa walipata nafasi ya kunadi sera na kujibu maswali matatu waliyoulizwa na wabunge kabla ya mchakato wa upigaji kura haujaanza, kisha kuchagua wawakilishi waliosimamia zoezi la kuhesabu kura zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live