Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nguvu mnayotumia kujadili Simba na Yanga itumieni kupima UKIMWI

WhatsApp Image 2021 05 11 At 14.47.29 660x400.jpeg Nguvu mnayotumia kujadili Simba na Yanga itumieni kupima UKIMWI

Tue, 11 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Mbunge wa Viti Maalum  (CCM),  Hawa Mchafu amedai baadhi ya wanaume wa Tanzania wanatumia nguvu kubwa kujadili habari za Simba na Yanga kuliko hata kujadili afya zao.

Hawa amesema kama nguvu hiyo ingetumika kujadili masuala ya afya ikiwemo kupima UKIMWI  huenda vita dhidi ya ugonjwa huo ingekuwa nyepesi.

Mbunge huyo ametoa kauli hiyo leo May 11, 2021  bungeni Dodoma wakati akichangia  hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya mwaka 2021/22.

“Wanaume ile nguvu mnayoitumia kujadili Simba na Yanga, Siasa na uke wenza ihamisheni ipelekeni kwenye masuala ya kupima virusi vya UKIMWI” Mchafu

Kuhusu ukeketaji, amesema wanaume wanatakiwa kutangaza hadharani kwamba hawawezi kuwaoa wanawake waliokeketwa lakini kukaa kwao kimya bado ukatili huo utaendelea.

Kwa mujibu wa Mbunge Hawa, wanaume wakisema ladha ya waliokeketwa ni tofauti na wasiokeketwa, jambo hilo litakwisha mara moja na kubaki historia.

Chanzo: millardayo.com