Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nec yapuliza kipenga majimbo 3

10259 NEC+PIC TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imetangaza uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo matatu na udiwani katika kata mbili, ikieleza kuwa uchaguzi huo utafanyika Septemba 16.

Majimbo hayo ni Korogwe vijijini ambalo aliyekuwa mbunge wake, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu alifariki, Ukonga na Monduli ambayo wabunge wake walijiuzulu na kuhamia CCM.

Akizungumza mjini Dodoma jana, makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Mbarouk Salim Mbarouk alisema fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 13 hadi 20, kampeni zitaanza Agosti 21 hadi Sptemba 15. “Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu tume uwapo wa nafasi wazi za ubunge katika majimbo matatu,” alisema.

Mwita Waitara (Ukonga) na Julius Kalanga (Monduli), walikuwa wabunge kwa tiketi ya Chadema lakini walijivua uanachama na kujiunga na CCM siku za hivi karibuni.

Pia, alisema tume inatoa taarifa kwa umma kuwa uteuzi, kampeni na uchaguzi wa madiwani wa Tindabuligi na Kisesa katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu uliohirishwa hapo awali nao utafanyika Septamba 16.

Wakati Nec ikitangaza hivyo, uchaguzi mdogo ubunge wa Buyungu unaotarajiwa kufanya Agosti 12.

Chanzo: mwananchi.co.tz