Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nec yamrejesha mgombea udiwani wa CUF ulingoni

20090 Pic+nec TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imemrejesha kuendelea kugombea udiwani wa Kibutuka wilaya ya Liwake mkoani Lindi, Mdohoma Ismaili kupitia CUF.

Taarifa ya Nec iliyotolewa leo Jumapili Septemba 30, 2018 na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Hamis Mkunga imeeleza kuwa tume ilipokea rufani ya Ismaili akipinga kuenguliwa kugombea kinyume cha taratibu.

Mkunga amesema tume katika kikao chake cha leo imekubaliana na maelezo ya mrufani na kuelekeza, “Arejeshwe kuendelea kuwa mgombea udiwani katika kata ya Kibutuka.”

“Halmashauri ya wilaya ya Liwale kwa kuwa imejiridhisha kwamba mrufani wakati wa kujaza fomu yake ya uteuzi Na. 8C alianza na jina la mwisho likifuatiwa na majina mengine kwa kuwa ndilo alilotaka lianze kuandikwa kwenye karatasi ya kupigia kura.”

Nec imesema Ismaili alienguliwa baada ya kuwekewa pingamizi na mgombea mwenzake kwa madai majina yake katika fomu ya uteuzi yalitofautiana na msimamizi wa uchaguzi kukubaliana na pingamizi hilo na hivyo kumuengua.

Mkunga anasema tume inavikumbusha vyama vya siasa na wagombea wanaoshiriki uchaguzi wa udiwani kwenye kata mbalimbali na ule wa ubunge wa Liwale utakaofanyika Oktoba 12, “Kuzingatia Sheria na Maadili ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani ya mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na hata siku ya uchaguzi.”

Chanzo: mwananchi.co.tz