Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai ni kama mganga anapokea wagonjwa, wale 19 sio Wabunge - Msekwa

MSEKWA NA WABUNGE WEB 660x400 Ndugai ni kama mganga anapokea wagonjwa, wale 19 sio Wabunge - Msekwa

Sat, 28 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

“Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha” Spika mstaafu Msekwa 

“Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba” Spika Mstaafu, Msekwa

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

ViaEATV.

HADHARANI MBOWE ASOMA BARUA WALIZOJIBU WAKINA HALIMA MDEE, BULAYA, MATIKO

Chanzo: millardayo.com