Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai azitaka sekta binafsi kuwa na uwazi kwa Serikali

77a7a426506b180b5cef7aca367f2b71 Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imedhamiria kuzishika mkono sekta binafsi nchini endapo zitafanya kazi na biashara zake kwa uwazi ikiwa ni pamoja na kulipa kodi kwa wakati.

Haya yamebainishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati akizungumza na wajumbe wa Chemba ya Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) na kusema kuwa Serikali inataka kuona sekta binafsi inakua kwa sababu inachangia pato la taifa

"Nadhani kitu pekee ambacho serikali inataka kutoka kwa sekta ya kibinafsi ni biashara ya uaminifu na wazi. Kuwa mkweli katika mwenendo wako unapofanya biashara, basi utapata msaada usio na masharti kutoka kwa serikali hii, nia ya Serikali ni ya dhati kwa maneno na vitendo vyake kwa sekta binafsi,” alisisitiza.

Ameongeza kusema kuwa ili bidhaa za Tanzania ziweze kushindana katika soko la dunia, sekta binafsi inapaswa kuzalisha bidhaa safi na salama zinazokidhi viwango vya kimataifa bila kusahau kufanya biashara ya uaminifu na uwazi ili taifa lipate fedha za kigeni.

Spika pia amezihaidi sekta binafsi kuwa zitaungwa mkono kikamilifu na Bunge kwani Bunge linafanya kazi kwa ukaribu na sekta hizo kwa kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

“Sisi wabunge tuko tayari kufanya kazi pamoja na TCCIA katika masuala ya sheria na sera kwa kutumia kamati yetu ya kudumu na mazungumzo ya mara kwa mara na kamati mbalimbali za kudumu za Bunge ili kukuza uchumi wa taifa,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live