Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai amwaga ‘madini’ kwa vijana

28209 Pic+ndugai TanzaniaWeb

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amewataka vijana nchini kuwa na mijadala inayofikia mwisho bila ya kugombana na waache kuanzisha malumbano yasiyokuwa na tija.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo Novemba 21, 2018 akifungua bunge la vijana lililoandaliwa na ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa kuwajengea uwezo wabunge awamu ya pili (LSP II).

Bunge hilo ambalo limejumuisha vijana kutoka vyuo vya elimu ya juu, alisema vijana wana wajibu wa kujadiliana kwa hoja bila ya kugombana au kuzodoana.

Amesema  vijana nchini wamekuwa na tabia ya kuanzisha mijadala mizuri, lakini mwisho wanaigeuza na kuwa malumbano ambayo hayafikii mwisho hivyo kuharibu maana nzima.

Ndugai amesema ni vyema vijana wakatumia mijadala kumaliza migogoro na migomo ambayo wanadhani ni suluhisho, ilhali inachochea uhasama.

"Ni matumaini yangu baada ya siku tano za bunge hili, vijana mtakuwa mmefikia malengo hayo, sisi tunawaombea na kuwatakia mafanikio makubwa katika kulijenga taifa lenu kuanzia sasa," amesema Ndugai.

Awali, akimkaribisha Ndugai, spika wa bunge hilo, Zephania Sane amesema matarajio yao ni kujifunza namna Bunge linavyofanya kazi hususan kupitisha miswada na kutungwa sheria za nchi.



Chanzo: mwananchi.co.tz