Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai akinzana na Rais Samia ?

IMGL2654 1140x640 1 Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: dar24.com

Jana Tarehe 27 Disemba 2021 Spika wa Bunge, Job Ndugai alihoji wanaofurahia nchi kukopa na kwamba deni limefika Sh70 trilioni, hii Leo Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni lazima serikali ikope ili kumaliza miradi ya maendeleo.

Akiwa katika mkutano mkuu wa pili wa wanakikundi cha Mikalile Ye Wanyusi uliofanyika jijini Dodoma, Spika wa Bunge Job Ndugai alitetea uamuzi wa Bunge kuanzisha tozo za miamala ya simu, kuliko kuendelea kukopa

Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe na kwa vipi” alisema Spika Ndugai.

“Tukasema pitisha tozo anayetaka asiye taka pitisha tozo, lazima tuanze kujenga wenyewe, nani atatufanyia, yuko wapi huyo mjomba, tukapitisha.

Ndugai aliongeza kuwa Juzi Rais Samia alikwenda kukopa Trilioni 1.3 na kusema Kuna siku nchi itapigwa mnada kwa kukopa.

“Sasa 2025 mtaamua mkitoa waliopo nayo sawa waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa, endapo hiyo ni namna ya kuongoza nchi, hivi sasa deni letu Sh70 trilioni hivi nyinyi si wasomi je hiyo ni afya?” Aliongeza Spika Ndugai

Chanzo: dar24.com