Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugai aiandikia barua NEC kujiuzulu mbunge wa Serengeti

20309 Ndugai+pic TanzaniaWeb

Tue, 2 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Spika Job Ndugai amepokea barua ya Marwa Chacha aliyejiuzulu ubunge wa Serengeti.

Marwa aliyejivunia uanachama wa Chadema Septemba 27,2018 alikuwa mbunge wa nne wa chama hicho kikuu cha upinzani kujiuzulu na kujiunga na CCM.

Wengine na majimbo yao katika mabano ni Mwita Waitara (Ukonga), Julius Kalanga (Monduli) na Dk Godwin Mollel (Siha).

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba Mosi, 2018 na ofisi ya Bunge inaeleza kuwa  Ndugai baada ya kupotea barua ya Chacha amemuandikia barua mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage  kumjulisha kuwa jimbo la Serengeti kuwa wazi.

“Kufuatia barua hiyo ya Spika, NEC inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge wa kujaza nafasi ya jimbo hilo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, kinaelekeza endapo mbunge atajiuzulu, atafariki au ataacha kazi ya ubunge kwa sababu nyingine yoyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113 cha sheria hiyo, Spika atamjulisha mwenyekiti wa NEC kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kiti hicho kuwa wazi.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz