Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchimbi awavaa CCM wanaopanga kuwapoteza wapinzani

Nchimbi Ccm (22).jpeg Nchimbi awavaa CCM wanaopanga kuwapoteza wapinzani

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amekemea kauli zinazotolewa na Vijana wa Chama hicho juu ya kuwapoteza Watu wanaowapinga akisema kauli kama hizo ni za kijinga.

Akiongea Jijini Mbeya leo Nchimbi amesema “Leo akiinuka Kijana wa CCM kwa mfano akasema Wapinzani wakifanya hivi na hivi lazima tuwapoteze huyu ni Kijana wetu lakini kasema jambo la kijinga tutalipinga na lazima tuone ni la kijinga kwasababu mwisho wa siku Nchi hii ni yetu sote”

Kauli ya Nchimbi inakuja siku moja baada ya jana April 16,2024 Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhan kutoa kauli iliyozua taharuki akiwa kwenye ziara katika Mji mdogo wa Rulenge Wilayani Ngara ambapo aliwataka Polisi wasihangaike kuwatafuta wanaotukana Viongozi pale watakapopotezwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live