Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi iongozwe kwa katiba wakati wote - Mbowe

MBOWE ApLS9.jpeg Freeman Mbowe

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema chama hicho kinatamani wakati wote nchi iongozwe na katiba iliyo bora ili kutengeneza ustawi ulio bora kwa wananchi wote.

"Tunaamini katiba iliyo bora itazaa sheria bora na vyote kwa pamoja vitatengeneza ustawi uliobora kwa raia wote, Nayazungumza haya nikiamini kwa muda mrefu katika nchi yetu kumekuwa na utamaduni wa walioko katika madaraka kuamini utashi wa kiongozi mkuu ndiyo unapaswa kuwa Dira ya Taifa.

"Dira ya Taifa letu wakati wote ili iwe ya haki kwa makundi na watu wote haipaswi kuwa utashi wa kiongozi mkuu, inapaswa kuwa imechimbiwa kwenyekatiba ya nchi,

Mbowe anetoa kauli hiyo leo Septemba 19, 2024 JiJini Dar es Salaam kwenyemkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) uliowakutanisha wadauku jadili tathmini ya hali ya demokrasia nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live