Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi inalitazama Jiji la Mbeya uchaguzi wa kesho

17546 SUGU+PIC TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' amesema nchi nzima inalitazama Jiji la Mbeya katika uchaguzi wa kesho Jumapili Septemba 16, 2018.

Amesema hiyo inatokana na msimamo wa wananchi wanaokikubali chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Septemba 15, 2018 katika mkutano wa mwisho wa kampeni za Chadema kata ya Maanga jijini Mbeya, kumnadi mgombea udiwani, Steven Mwashilindi.

“Ndugu zangu tutatia aibu kama CCM wakituchakachua Mbeya mjini katika uchaguzi wa kesho,” amesema Sugu.

“Katika uchaguzi huu nchi nzima inalitazama jiji la Mbeya. Wananchi msiogope lolote, twendeni tukapige kura na tukae mita 100 kulinda kura zetu.”

Amesema Chadema na wapenda mabadiliko wa Mbeya wana kila sababu ya kuiondoa CCM madarakani na mchakato huu ndio umeuanza sasa.

Kwa upande wake, Mwashilindi amewaomba wakazi wa Maanga kutofanya makosa, wamchague ili awatumikie.

 “Ninakwenda kukaa meza moja na meya wa Jiji hili ambaye anatoka Chadema. Ni rahisi kwangu kumshawishi katika kutekeleza miradi iliyopo ndani ya kata yetu.” Amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz