Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nasikia kuna Mabaunsa, Hakuna Baunsa mbele ya serikali’- Mambosasa

3429 Screen Shot 2017 10 24 At 6.39.47 PM 1024x577 660x400.png

Mon, 26 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo February 16, 2018 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Lazaro Mambosasa amewataka wananchi kujiepusha na vitendo vya kihalifu ili waweze kuruhusu uchaguzi wa marudio ufanyike kwa amani na utulivu.

“Jeshi la Polisi limejipanga vizuri, uchaguzi uliopita 2015, tulikuwa na majimbo kadhaa ndani ya DSM lakini kwa huu wa marudio tuna jimbo moja na kwa sababu hiyo ni seme kwamba Jeshi la Polisi tumejipanga imara na kuhakikisha hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingia na kufanya vurugu kwenye uchaguzi” -Mambosasa 

“Nimeambiwa kwamba kuna Mabaunsa lakini sijawahi kuona Baunsa anayeweza kupambana na Serikali halafu akabaki na Ubaunsa wake. Namuonea huruma huyo Baunsa aliyejiandaa kupambana na dola, niwashauri tu kuwa mtu haishi kwa kifua kikubwa bali anaishi kwa kutii sheria”-Mambosasa

Polisi DSM, kuhusu Kiongozi wa CHADEMA aliyenyongwa



 

Chanzo: millardayo.com