Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu meya Ilala ajiuzulu

9461 KUMBI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Diwani wa Kata ya Vingunguti (CUF), Omary Kumbilamoto ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Ilala amejizulu uanachama wa chama hicho.

Amechukua uamuzi huo jana Julai 31, 2018 huku akieleza kuchoshwa na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya CUF.

CUF kimekumbwa na mgogoro tangu mwaka 2016 baada ya kurejea kwa Profesa Ibrahim Lipumba ambaye mwaka 2015 alijiuzulu uenyekiti wa chama hicho kutokana na kutofautiana na viongozi wenzake.

Kumbilamoto  ameufananisha mgogoro huo wa CUF na mvutano wa mataifa ya Palestina na Israel, akieleza kuwa hauna suluhu na unamfanya ashindwe kuwatumikia ipasavyo wananchi wa Vingunguti.

Amesema amekuwa akipewa vitisho vya kufukuzwa uanachama kwa sababu ya hatua yake ya kuwa karibu na viongozi wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema wakati kata ya Vingunguti ikikumbwa na mafuriko,  hakuna kiongozi yoyote  wa CUF aliyekwenda kutoa msaada isipokuwa Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Sikuletewa hata kijiko na viongozi wangu wa chama  lakini viongozi wa Serikali walinisaidia. Hata hivyo, upande chama kinadai mimi ni msaliti kutokana na ushirikiano ninaoupata,” amesema Kumbilamoto.

Amesema wakati wowote atafanya mkutano wa hadhara wa kueleza wa wananchi wa kata hiyo wapi atakapoelekea kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa.

Akizungumza na MCL Digital kuhu uamuzi wa Kumbilamoto, meya wa Ilala, Charles Kuyeko amesema,“ nimesikia kama ulivyosikia wewe, lakini hajaniaga na wiki nzima nilikuwa namtafuta simpati.”

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz