Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Spika akerwa na wabunge wanaopiga kelele

TULIIIIAAAA 11 Naibu Spika akerwa na wabunge wanaopiga kelele

Thu, 17 Jun 2021 Chanzo: eatv.tv

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, ameonesha kutokufurahishwa na jinsi ambavyo wabunge wa Bunge hilo wanavyopiga kelele ndani ya Bunge hata kama kuna mwenzao anatoa hoja.

Submitted by Agnes Kibona on Alhamisi , 17th Jun , 2021 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson

Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo leo Juni 17, 2021, Bungeni Dodoma wakati wa majadiliano ya Bajeti, na kueleza kuwa hali hiyo imekuwa ikijirudia mara kwa mara na kwamba kuanzia leo ataanza kuwachukulia hatua.

"Waheshimiwa wabunge mliosimama naomba mkae, wabunge mnapiga kelele sana mimi huletewa malalamiko lakini huwa sipendi sana kuwaambia keleleni, sababu watu wanasikiliza na wamekuja hapa Bungeni kujifunza, tujizuie kuongea kwa sauti kama upo nje, pia anayechangia hapa wewe msikilize ili hoja uielewe," amesema Dkt. Tulia.

"Kuna wengine mnaenda kwenye kile kiti (Kwa Waziri Mkuu), yeye atasikiliza saa ngapi hoja za wabunge? na yeye ndiyo msimamizi wa shughuli za serikali Bungeni kwa hiyo tafadhali, sasa hivi nikiona mtu pale amekaa muda mrefu nitakunyanyua," amesisitiza Dkt. Tulia.

Chanzo: eatv.tv