Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Spika akemea utovu wa nidhamu Bungeni

ZUNGU WEB Naibu Spika, Mussa Azan Zungu

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Spika, Mussa Azan Zungu amewaonya wabunge kuzingatia nidhamu pamoja na kuacha kuwakatisha wachangiaji kwa kutoa taarifa ambazo nyingi hazina msingi bali zinamtoa mbunge kwenye mtiririko wake.

“Kuanzia mjadala wa bajeti kuu hapatakuwa tena na taarifa za mchezo humu ndani. Hivi karibuni wabunge wamekuwa wakilalamika mnawaingilia flow [Mtiririko] zao za kuchangia, taarifa zimekuwa nyingi si taarifa za maana, bali taarifa za kupotezeana muda,” amesema.

Hata June 14 Bunge litajadili Bajeti Kuu ambayo itakuwa ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live