Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naibu Msajili avitaka vyama vya siasa kuiga mfano wa ACT-Wazalendo

ACT.jpeg Naibu Msajili avitaka vyama vya siasa kuiga mfano wa ACT-Wazalendo

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema vyama vingine vya siasa kuiga mfano wa chama cha ACT- Wazalendo kwa kuwa na ofisi ya kisasa ya makao makuu, akisema wamepiga hatua kubwa.

Nyahoza ametoa kauli hiyo, jana Jumapili Oktoba 30, 2022 wakati alipohudhuria uzinduzi wa ofisi ya makao makuu ya ACT-Wazalendo iliyopo eneo la Magomeni Usalama wilayani Kinondoni.

"Tunafarijika kama Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, na mimi nimeingia hii ofisi nitoe wito vyama vingine muige hili, ila mjitahidi muweze kukamilisha usajili ambao kisheria ni siku 14 ili msije kuwa kama mtu anayenunua gari alafu halina usajili anabaki kulipaki tu" Alisema Nyahoza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live