Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC yawataka wananchi wajitokeze kuchagua madiwani

37326 Pic+nec+masiwani NEC yawataka wananchi wajitokeze kuchagua madiwani

Sun, 20 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa kata tatu, uliopangwa kufanyika kesho Jumamosi Januari 19, 2019.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika katika kata ya Magomeni kwenye halmashauri ya manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kata ya Mwanyahina iliyopo halmashauri ya wilaya ya Meatu mkoani Simiyu na kata ya Biturana katika halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma.

Akizungumza leo Ijumaa Januari 18, 2019 Mwenyekiti wa Tume, Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage amesisitiza watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliojiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Amesema wananchi wajitokeze kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi kilichobaki kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Jaji Kaijage amesema jumla ya wapiga kura 26,282 katika vituo vya kupigia kura 69 watahusika na uchaguzi huo mdogo wa udiwan na kuwaasa viongozi wa vyama vya siasa, wagombea, wafuasi wao na wananchi kwa ujumla wajiepushe na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu wakati wa uchaguzi.

“Pale panapokuwa na malalamiko yoyote ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za uchaguzi, malalamiko hayo yawasilishwe kwenye mamlaka inayohusika kwa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Jaji Kaijage amesema upigaji kura utafanyika katika vituo vilevile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuongeza kwamba vituo vitafunguliwa kuanzia saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (12:00) jioni.

“Iwapo wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari, ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura. Mlinzi  wa kituo cha kupigia kura, atasimama nyuma ya mpiga kura wa mwisho aliyekuwepo kituoni kabla ya saa 10 jioni.”

“Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya muda huo,” ameelekeza Jaji Kaijage.



Chanzo: mwananchi.co.tz