Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC yawapiga msasa wasimamizi wa uchaguzi

Kuraaa.png NEC yawapiga msasa wasimamizi wa uchaguzi

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata kuzingatia sheria wakati wa kutelekeza majukumu yao ili uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 23 ufanyike kwa ufanisi.

Kauli hiyo imetolewa na Mjumbe wa NEC Jaji Asina Omari wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi ngazi ya jimbo na kata zinazotarajia kufanya uchaguzi mdogo wa madiwani Machi 20, 2024.

Amesema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa uchaguzi kuwa mzuri na wenye ufanisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live