Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC yawahimiza wasimamizi kutenda haki chaguzi ndogo

Efae0c0bf73939676171706434ba20a2.png NEC yawahimiza wasimamizi kutenda haki chaguzi ndogo

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanasimamia taratibu za uchaguzi ili haki itawale.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Emmanuel Kavishe wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka katika majimbo ya Bumbuli, Same na Monduli yanayofanyika mkoani Tanga.

Alisema kuwa wanajukumu la kuhakikisha wanafanikisha chaguzi ndogo zinatarajiwa kufanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi mnamo Mwezi Mei.

"Niwaase acheni kufanya kazi kwa mazoea au kufanya upendeleo kwa watu fulani au chama fulani, mkahakikishe mnakwenda kusimamia chaguzi zinafanyika katika misingi ya uhuru na haki," alisema Kavishe.

Hata hivyo Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga, Sebastiani Masanja aliwataka kuzingatia maelekezo watakayopewa katika mafunzo hayo kwani watakwenda kuyafanyia kazi kipindi cha uchaguzi utakapofika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz