Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC yatembelea Kata ya Mlowa kujionea maandalizi ya uchaguzi

11099 NEC+PIC TanzaniaWeb

Thu, 9 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ametembelea Kata ya Mlowa Bwawani halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kushuhudia maandalizi ya uchaguzi mdogo wa udiwani.

Ameitembelea Kata hiyo leo Alhamisi Agosti 9, 2018 na kuzungumza na wasimamizi wa uchaguzi na ofisa uchaguzi wa jimbo la Mtera, Elizabenth Gumbo.

Jaji Mbarouk ameridhishwa na maandalizi na kuwataka  wasimamizi wa uchaguzi wa Kata hiyo kutumia vipaza sauti kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa maelezo kuwa njia hiyo itarahisisha kufikisha ujumbe kwa wananchi wengi zaidi.

Akitoa taarifa ya maandalizi ya uchaguzi, Elizabeth amesema yanakwenda vizuri na tayari wamepokea vifaa vya awali ikiwemo mfano wa karatasi ya kupigia kura, mabango na fomu za uchaguzi, bahasha za karatasi za kura na fedha za bajeti ya uchaguzi.

Amesema wameshatoa taarifa kwa  vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya mawakala wao kwa ajili ya taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na kuwaapisha.

Amebainisha kuwa changamoto iliyopo katika kampeni kwenye Kata hiyo ni kuhusu mabadiliko ya ratiba ya kampeni za CCM na Chadema kutokana na chama kimoja kukataa kubadili ratiba yake ya kampeni.

Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Kata hiyo, Cleopa Leuna amesema kuna vituo 19 vya kupigia kura na k12 vipo kwenye maeneo ya wazi na vinahitaji kujengewa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz