Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC yatangaza tarehe ya uchaguzi kata 13

69652 Pic+nec

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 13 za Tanzania Bara utakaofanyika Agosti 17, 2019.

Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa jana Ijumaa Agosti 2, 2019 inaeleza kuwa utoaji wa fomu za wagombea ulipangwa kuanza Julai 29 hadi leo Jumamosi Agosti 3, 2019 ambapo pia utafanyika uteuzi wa wagombea.

Inaeleza kuwa hadi jana saa 10 jioni wagombea 58 wa vyama vya siasa 18 walichukua fomu za uteuzi.

Vyama ambavyo wagombea wake wamchukua fomuĀ  na idadi yao katika mabano ni Demokrasia Makini (5), AAFP (5), CCK (3), DP (4), SAU (4), UDP (4), ACT-Wazalendo (2), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), Ada Tadea (4), Chadema (2), Chaumma (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2) na UMD mmoja.

Chanzo: mwananchi.co.tz