Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata 23 za Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima Ramadhani jijini Dodoma leo Alhamisi Februari 15, 2024 uchaguzi huo utafanyika Machi 20, 2024.
Taarifa inaeleza kuwa, kata zitakazofanya uchaguzi huo mdogo ni Kimbiji iliyo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti), Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).
Nyingine ni Isebya iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Mshikamano (Halmashauri ya Wilaya ya Musoma), Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Nkokwa (Halmashauri ya Wilaya ya Kyela), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu) Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.