Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC kuja kidigitali zoezi la uandikishaji

Kuraaa.png NEC kuja kidigitali zoezi la uandikishaji

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini (NEC) imekutana na wadau wa uchaguzi mkoani Tabora ikiwa ni hatua ya mapema katika maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura .

Akizungumza na wadau hao wa uchaguzi mkoani Tabora kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) Mtibora Selemani amesema tume hiyo kuanzia Novemba 24 mpaka 30,2023 itaanza majaribio ya uandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo litahusisha kutumika kwa vifaa vyenye teknolojia ya kisasa lengo ikiwa ni kupima ufanisi wa vifaa hivyo kabla ya zoezi hilo kuanza kwa nchi nzima .

Tume hiyo ya uchaguzi imesema zoezi hilo la majaribio linafanyika katika mikoa miwili nchini kwa maana ya mkoa wa Tabora na Mara likihusisha vituo 16 katika kata mbili za mikoa hiyo ambapo kwa Tabora litafanyika katika kata ya Nga’mbo iliyopo katika manispaa ya Tabora na kata Ikoma iliyopo wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Mkurugenzi wa idara ya daftari na TEHAMA Geofrey Mpangala akieleza kuhusu kutumika kwa teknologia mpya za kisasa katika zoezi la uandikishaji amesema mapinduzi hayo yamelenga kwenda kulifanya zoezi la uandikishaji kuwa rahisi zaidi pamoja na kuokoa muda kwa wananchi wakati wa zoezi hilo huku wadau wa uchaguzi wakiishukuru tume ya uchaguzi kwa kuja na maono hayo ya kiteknologia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live