Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NEC kuboresha kwa majaribio daftari la kudumu la wapiga kura

NEC Kuboresha Kwa Majaribio Daftari La Kudumu La Wapiga Kura NEC kuboresha kwa majaribio daftari la kudumu la wapiga kura

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kufanya zoezi la uboreshajia wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura katika kata ya Ng’ambo iliyopo Mkoani Tabora na kata ya Ikoma iliyopo Mkoani Mara kuanzia Novemba 24 hadi 30 mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 10,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uboreshaji wa majaribio wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Bw. Kailima amesema zoezi hilo la uboreshaji litafanyika katika vituo 16 vya kuandikisha wapiga kura kati ya hivyo vituo 10 ni katika kata ya Ng’ambo na 6 vipo kata ya Ikoma.

“Uboreshaji wa majaribio utahusisha kuandikisha raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 au zaidi na atakayetimiza umri wa miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 , wapiga kura wanaoboresha taarifa zao ambao wamehama kutoka eneo moja la uchaguzi kwenda eneo jingine, wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo daftarini,”amesema Bw. Kailima.

Aidha, ametaja lengo la kufanya zoezi hilo kuwa ni kupima uwezo wa vifaa na mifumo ya uandikishaji itakayotumika wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaotarajiwa kufanyika nchi nzima kwa tarehe na ratiba itakayopangwa na tume.

“Katika zoezi hili tume itatumia BVR Kits zenye vifaa mbalimbali vinavyowasiliana ili kuchukua na kutunza taarifa za wapiga kura, BVR Kits hizo zimeboreshwa na ni tofauti na zile zilizotumika katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 na 2019,”amesema Kailima.

Katika hatua nyingine Bw.Kailima amesema kuwa uboreshaji huo utahusisha vyama vya siasa kwa kuweka wakala mmoja katika kila kituo cha kuandikisha wapiga kura lengo likiwa ni kushuhudia na kujiridhisha kuhusu taratibu zitakazotumika wakati wa uboreshaji wa majaribio wa daftari.

Amesema utaratibu huo wa uboreshaji wa taarifa kwa njia ya mtandao hautawahusisha wapiga kura wapya wanaotaka kuandikishwa kwa mara ya kwanza na waliopoteza kadi zao au kuharibika.

“Hawa wanashuriwa wafike kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura na kufuata taratibu watakazo elekezwa na maafisa wa Tume watakaokuwepo kwenye kituo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live