Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NCCR Mageuzi yajitosa uchaguzi wa marudio

IMG 20221028 WA0309 NCCR Mageuzi yajitosa uchaguzi wa marudio

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza uchaguzi wa marudio katika jimbo la Amani visiwani Zanzibar na nafasi za madiwani kwenye kata 12 za Tanzania Bara, Chama cha NCCR-Mageuzi kimeshawishi wanachama wake kushiriki kwa kufuata utaratibu uliotangazwa.

NEC imepanga marudio ya uchaguzi huo siku tano zijazo baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mussa Hassan (CCM) kufariki Dunia Oktoba 13, mwaka huu.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kushiriki uchaguzi bila James Mbatia aliyefukuzwa uanachama hivi karibuni akiwa ametumikia nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho kwa miaka kadhaa.

Akizungumza na wanahabari leo Novemba 12,2022 jijini Dar es Salaam, Makamu mwenyekiti wa chama hicho, Joseph Selasini amesema ni nafasi nzuri kwa chama kuonyesha kinafanya kazi zake.

“Wale wenye propaganda NCCR Mageuzi haipo, watatuona kwenye kampeni na hatuendi kushiriki tu tunakwenda kushindwa, tutafanya vizuri,”alisema Selasini.

Alisema wagombea kupitia chama hicho walifanya vizuri katika baadhi ya kata hizo kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, hivyo hakuna sababu ya kutoshiriki.

Chanzo: Mwananchi