CHAMA cha NCCR Mageuzi kimeipongeza serikali kuingia mkataba na DP World kuwa una manufaa zaidi kwa watanzania kwani serikali inapata asilimia 60 na DP World inapata asilimia 40.
Akizungumza Makao Mkuu ya Chama hicho Ilala jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, Joseph Selasini amesema wao kama NCCR waliitikia wito wa Rais Samia Suluhu Hassan na kiungwana uwezi kugomea wito wa Rais wa nchi.
“Mwaliko umekuja sio jukumu letu kuhoji mualiko umekujaje au kwa nini nimealikwa, unachopaswa kufanya ni kuitikia mwaliko na kwenda kusikiliza na kuchambua yale unayoelezwa.”Amesema Selasini na kuongeza
“Utafanya maamuzi kulingana na ufahamu wako na vile unavyoweza kuelewa, uwezi kupewa mwaliko na Rais ukaukataa, ndio maana tuliudhuria na wengine waliudhuria, kuwe na ajenda kusiwe na ajenda au ajenda yenye mashaka, hoja ya kiungwana uwezi kukataa wito, kata maneno sio wito.”Amesisitiza
Amesema kuongoza ni kuvumilia, kiongozi mzuri lazima aonyeshe kiwango cha juu cha uvumilivu.
“Baada ya mkataba wa awali IGA kupitishwa bungeni watanzania na taasisi nyingi zikiwemo za dini walilalamika na kutoa maoni mbali mbali;…… ““Mkataba wa awali haufanani na mkataba kamili, IGA ni mkataba wa awali.”Amesema na kuongeza
“Tunataka serikali itengeneze timu ya kufaa ya wazalendo watakaofuatilia kwa maslahi ya Watanzania utekelezwaji wa mkataba wa DP World, kama mkataba wa DP World utatekelezwa utakuwa na faida kubwa sana kwa Watanzania.”Amesema Selasini -