Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

NCCR Mageuzi wafunguka chanzo cha mgogoro, Selasini atajwa

Nccrrr123IMG 0133.png Simbeye akizungumza

Tue, 24 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Idara ya Uenezi na Uhusiano ya Umma wa NCCR Mageuzi, Edward Simbeye amefunguka kwa kina kuhusu chanzo cha mgogoro ndani ya chama hicho.

Akizungumza katika kipindi cha Front page kinachorushwa na Kituo cha Redio cha +255 Global Radio, Simbeye amesema chanzo cha mgogoro huo, ni baadhi ya wanachama kuvunja katiba ya chama hicho.

Akizungumzia tuhuma zilizoibuliwa na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Martha Rafael Chiomba kwamba alilazimishwa kuondoka madarakani ndani ya chama hicho na viongozi wa juu, Simbeye amesema vyama vyote vya siasa vinaongozwa na katiba na siyo maneno.

Amesema katibu mkuu huyo alifanya makosa kwa kutoa tuhuma kwenye vyombo vya habari badala ya kufuata taratibu za chama ambapo baada ya kuona tuhuma hizo, chama hicho kiliitisha mkutano Mei 15, 2022 kwa lengo la kumhoji kuhusu tuhuma alizozitoa, ambapo alikiri kufanya makosa.

Ameongeza kuwa, Chiomba alifikia hatua ya kuibua tuhuma hizo baada ya kugundua kwamba yeye na wenzake, akiwemo Joseph Selasini walifanya makosa ya kukiuka msimamo wa chama wa kugomea kushiriki kwenye mkutano wa Kituo cha Demokrasia (TCD) uliofanyika jijini Dodoma.

Amesema katika kikao cha Kamati Kuu ya NCCR kilichofanyika April 4, mwaka huu, kilitoka na maazimio ya chama hicho kutoshiriki mkutano wa TCD lakini katibu mkuu huyo na wenzake, wakaenda kuhudhuria kinyume na utaratibu, alipoona atachukuliwa hatua ndipo alipoibuka na tuhuma hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live