Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Makamba awaonya wanaoutaka Urais 2025

MZEE MAKAMBA Mzee Makamba

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan atawabatiza wananchi kwa maji na faraja.

Makamba ametoa kauli akimuombea kura mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Abdulrahman Kinana katika Mkutano Mkuu Maalum wa CCM unaoendelea Dodoma huku akiwaonya wale wanaonyemelea kiti cha urais mwaka 2025.

"Wanasema mzigo mzito mpe Mnyamwezi, lakini usiogope Rais, kama mzigo mzito aliubeba Mkwere vipi Mzanzibar aushindwe? Nakuombea (Rais Samia) uwe na mabega makubwa ya kuubeba mizigo mzito.

"[Mwaka] 2025 mgombea ni wewe [Samia Suluhu Hassan]. Kama kuna anayejiandaa huko, akae tayari.

"Mimi na Kinana tuliitwa Kamati ya maadili ya CCM na wengine walisema maneno lakini tulisamehewa. Kwa kuwa Kinana utakuwa boss wao usije kusema sasa na mimi nilipize, Kinana samehe.

"Nelson Mandela alisema msamaha ni silaha ya watu imara, na watu imara hawaogopi kusamehe kwa ajili ya watu na maendeleo. Mimi na Kinana tulinyeshewa na mvua ndani ya CCM, Kinana samehe.

“Kinana tuna ligi 2025 na tunataka kushinda, hatutaki kumwachia mtu mwingine hii nchi. Usiogope kwani unakuja kulima? Maneno ya CCM yapo kwenye katiba na yanatekelezeka.

"Ulipoachaguliwa rafiki yangu Gwajima aliniambia wewe ni mtabiri wa CCM, kufuatia uongozi wa Mama Samia unatabiri nini, maana kwa Magufuli ulitabiri kuwa utakuwa ubatizo wa moto nikasema, chini yako mama utakuwa ni ubatizo wa maji na faraja.

"Kwa utaratibu wa jeshi mkiwa Kanali na Luteni, Kanali anakaa mbele, lakini mimi na Kanali Abdulrahman Kinana tulisafiri wiki nzima akaniambia hayo mambo jeshi sawa, lakini wewe kaa mbele. Kinana ni sio mtu wa kujikweza," amesema Makamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live