Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee Makamba: Kinana wasamehe waliokupiga madongo

Makamba Kinana.png Mzee Makamba na Kinana

Fri, 1 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Yusuph Makamba, amemtaka Abdulrahman Kinana, atakapopitishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, asitumie madaraka yake kulipa kisasi kwa watu waliompiga madongo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mwanasiasa huyo mkongwe nchini Tanzania, ametoa ombi hilo leo Ijumaa, tarehe 1 Aprili 2022, akiwaomba Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, wampitishe katika nafasi hiyo aliyopendekezwa kugombea jana na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

“Watu dhaifu hawaweziu kusamehe usije tena ukaondoka hapa, jamani mliniita kamati kuu sasa mimi ndiyo makamu mwenyekiti mtaniona, hapana, yameisha.Nawaombeni ndugu zangu zawadi ambayo tunaweza kumpa Kinana leo ni kura,” amesema Mzee Makamba.

Mzee Makamba amesema, yeye na Kinana walipitia misukosuko ndani ya CCM, kiasi cha kufikishwa kuhojiwa mbele ya Kamati ya Maadili ya chama hicho, kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.

Kufuatia mazungumzo yao ya kukosoa kitendo cha CCM kukaa kimya, dhidi ya watu wanaokosoa wastaafu.

“Mimi nimenyeshewa mvua humu ndani ya CCM, najua mwenyewe, nikakaukia kwa Jakaya Kikwete. Mimi na mwenzangu Kinana tuliikishwa kwenye maadili na tukasamehewa na hata wako waliokuwa wamesimama wakatutupiua madongo,” amesema Mzee Makamba.

Tarehe 10 Februari 2020, Mzee Makamba na Kinana walifika kuhojiwa mbele ya Kamati Ndogo ya Usalama na Maadili ya CCM , kwenye ofisi ndogo za chama hicho Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuhojiwa na kamati hiyo, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), ilimsamehe Mzee Makamba na kumpa onyo Kinana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live