Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwitikio wa Chadema kwenye maandamano wazua maswali

Lissu Maandamano AZL7R.jpeg Mwitikio wa Chadema kwenye maandamano wazua maswali

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zikiwa zimepita siku 11 tokea Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe atangaze maandamano yaliyohitimishwa leo,mwitikio wake umewasikitisha wananchi wengi na kuhoji chama hicho kinapoelekea tofauti na nguvu iliyokuwa nayo miaka 10 iliyopita

Wakizungumza katika maeneo tofauti yalipopita maandamano hayo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar esSalaam,walieleza kuwa mwitikio mdogo wa wananchi si kiashiria kizuri cha maendeleo ya Chadema katika kuwashawishi wananchi kama walivyokuwa zamani

Mustapha Morie Mfanyabiashara wa Matunda katika soko la Buguruni, alieeleza kuwa hakutarajia mwitikio mdogo wa wananchi katika maandamano hayo yaliyoongozwa na viongozi wa kitaifa wa Chadema

Mimi nilijua baada ya serikali kuruhusu maandamano wananchi wengi wangejitokeza kwa kuwa miaka kadhaa nyuma chama hiki kilipoitisha maandamano licha ya kuzuiwa kwa nyakati tofauti lakini uungwaji mkono ulikuwa mkubwa kuliko hivi sasa”alisema Morie.

Dereva wa boda boda Mjulusi Mganza aliyejitambulisha kuwa anatokea kituo cha Buguruni Malapa,alisema kilichomsukuma kushiriki na kubeba bendera ya chama hicho katika maandamano hayo ni malipo na mafuta aliyopatiwa kwa makubaliano ya kuishia katika kituo cha Manzese

Aliongeza kuwa katika hali ya kawaida usafiri wa mara moja wa kutoka Buguruni Malapa kwenda Manzese haifiki shilingi 14,000 na kutaja kiasi hicho ndicho alichopokea kwa sharti la kuingiza pikipiki yake kwenye maandamano.

“Nilidhani tutakuwa wengi katika hili mimi ninaishia Manzese Darajani hii bendera nasepa nayo hata wenzangu nadhani nao wataishia hapo hapo kwa kuwa kijiweni kwetu mkataba ulitutaka tuishie Manzese”alisema Mganza

Mariam Stephano Mkazi wa Kimara Baruti alisema kilichomvutia kushiriki maandamano hayo ni ngoma zilizokuwa zikipigwa maarufu kigoma cha Uruguay.

“Wala sikuwa na taarifa nikaona watu wanapita na ngoma akiwemo shoga yangu Mwajey namuuliza ananiambia twende twende name nikaunga baadae ndiyo tukakutana na Lissu pamoja na Mbowe lakini sijafika mpaka mwisho”alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live