Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwita Waitara aibuka na ilani ya CCM jimboni Buyungu

9746 WAITARA+PIC TanzaniaWeb

Thu, 2 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kakonko. Kada wa CCM Mwita Waitara amesema ilani ya CCM imeonyesha dhamira ya dhati ya kutekeleza kwa vitendo ahadi inazozitoa katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Akizungumza leo Agosti 2 kwenye kijiji cha Itumbiko wakati wa mkutano wa hadhara wa kumnadi Mgombea ubunge wa jimbo la Buyungu (CCM) Christopher Chiza Waitara amesema kuwa ilani ya CCM ndiyo injini ya usimamizi wa maendeleo ya nchi.

Julai 29 Waitara alitangaza kujiuzulu ubunge na uanachama Chadema na kuhamia CCM.

Akizungumza katika mkutano huo amesema atatumia nguvu zote kuitangaza ilani ya CCM kwa maisha yake kwani ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi.

“Maendeleo ya nchi yamebebwa na ilani ya CCM na ndiyo yenye serikali inayotekeleza ilani hiyo kwa sasa na kwamba utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo chini ya usimamizi wa Raisi John Magufuli imezingatia utekelezaji wa ilani,” amesema

Akitoa mfano wa hilo ameeleza kuwa katika ukurasa wa 67 ilani inaeleza namna mgombea wa CCM atakavyoimarisha viwanja vya ndege nchini kazi ambayo anaifanya sasa.

Kwa upande wake, aliyekuwa mbunge wa Moshi vijijini, Dk Cyril Chami amewaonya wananchi wa jimbo la Buyungu kutochagua wabunge wenye tabia ya kususia vikao ikiwamo bunge maalum ambalo Raisi anahutubia kwani kufanya hivyo ni sawa na kupishana na gari la fedha.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz