Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwita Waitara aibuka kidedea Ukonga

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Ukonga, Jumanne Shauri amemtangaza mgombea wa CCM, Mwita Waitaka kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana.  

Akitangaza matokeo hayo leo asubuhi Septemba 17, 2018 katika ukumbi wa Anatoglo jijini humo amesema Waitara amepata kura 77,795 sawa na asilimia 89.19 na mshindi wa pili ni Asia Msangi wa Chadema aliyepata kura 8,676 sawa na asilimia 9.95.

Amesema uchaguzi huo ulishirikisha vyama 14.

Shauri amesema watu waliotarajiwa kupiga kura walikuwa 300,609 lakini waliojitokeza ni watu 88,270 sawa na asilimia 29.4

Wakati matokeo hayo yanatangazwa ulinzi umeimarishwa nje ya kituo, polisi wamewekwa kwenye milango ya kuingilia na njia ilifungwa kwa muda.

Ndani ya ukumbi hali ilikuwa tulivu na baada ya kutangazwa, Mwita alipongezwa kwa kupewa mkono. Hakukuwa na ushangiliaji sana na mchakato huo umekamilika.

Chanzo: mwananchi.co.tz