Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwinuka wa CCM mshindi kata ya Mwanganyanga

11555 UCHAGUZI3+PIC TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kyela. Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mwanganyanga wilayani Kyela jijini Mbeya, Alex Mwinuka ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 867, akiwabwaga wapinzani wake wa vyama vinne vilivyoshiriki uchaguzi huo.

Mwinuka ametangazwa leo Jumapili Agosti 12, 2018 na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kyela, Francis Mwaipopo.

Mwaipopo amewataja wagombea wengine kuwa ni Kanyiki Andembwisye (Chadema) kura 748, Amani Mwaijeja wa CUF (24), Danford Mwambije (ACT-Wazalendo) kura 16 na Wilson Mwakilasa wa NCCR-Mageuzi (14).

Amesema katika uchaguzi waliojiandikisha kupiga kura ni 2,696 na waliopiga kura wakiwa 1,699 na kubainisha kuwa kura halali zilikuwa 1,687 na 29 ziliharibika.

Hata hivyo, wagombea wa Chadema, CUF na ACT-Wazalendo waligoma kusaini fomu ya matokeo ya jumla kwa madai kuwa msimamizi wa uchaguzi huo ametumia mabavu kuwahujumu kwa kuwataka wasaini matokeo ya jumla wakati hayajajumlishwa.

Kanyiki amesema, “kwanini unatulazimisha tusaini tusichokijua, matokeo hayajajumlishwa halafu unatuambia tusaini kweli. Kwanza baadhi ya mawakala wetu wamenyimwa nakala za fomu za matokeo.”

“Mnachotufanyia si demokrasia kabisa, tumeporwa haki zetu.”

Hata hivyo, msimamizi huyo amesema matokeo yote yamejumuishwa kwenye vituo vya kupigia kura na kila mgombea kupitia kwa wakala wake amepewa nakala hivyo madai hayo hayana msingi ingawa aliwataka wafuate sheria nyingine zinavyoelekeza.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz