Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema ajiuzulu, arejea CCM

11399 MWENYEKITI+PIC TanzaniaWeb

Sat, 11 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Monduli. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli wa Chadema, Isaack Joseph amejiuzulu na kujiunga na CCM.

Joseph ambaye aliyekuwa diwani wa Monduli mjini, ametangaza uamuzi huo leo Agosti 11 katika kikao cha baraza la madiwani.

Akizungumza baada ya kutangaza uamuzi huo, Joseph amesema anaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuwaletea maendeleo  wananchi.

"Nimefanya uamuzi huu kwa sababu mambo mengi ambayo upinzani waliahidi kufanya sasa yamefanywa na Magufuli sasa hakuna sababu ya kupingana na maendeleo ," amesema.

Joseph ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa madiwani wa Chadema Kanda ya Kaskazini ameema anataka kushirikiana na Serikali.

Mwenyekiti huyo alijiunga na Chadema mwaka 2015, baada ya kujiuzulu nafasi katibu mwenezi wa CCM Mkoa Arusha ili kumfuata Lowassa alipotangazwa kugombea Urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz