Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti ajilipua madeni Jumuiya ya Wazazi CCM

30414 Ccm+pic Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa

Thu, 6 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Dk Edmund Mndolwa amesema yupo tayari kuacha kazi kama atashindwa kuiongoza jumuiya hiyo kulipa madeni.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule na makatibu wa jumuiya hiyo wilayani Moshi. Alisema bado jumuiya ina madeni makubwa yanayotokana na shule zake 55.

Mndolwa, ambaye hakutaka kuweka wazi kiasi cha madeni hayo, alisema katika utawala wake, lazima yalipwe.

“Inasikitisha kuona watu wazima wanadaiwa halafu wananyamaza. Kama itabidi tuuze shule ili tulipe madeni tutafanya hivyo, lakini watu wazima hatuwezi kuwa na deni tukakaa tu,” alisema Mndolwa.

“Anaingia mwenyekiti huyu kuna madeni, anatoka mabilioni hayajalipwa, haiwezekani, katika utawala wangu. Sitatoka na deni.”



Chanzo: mwananchi.co.tz