Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti UVCCM ataja sababu wagombea CCM kutokubalika

60573 Uvccm+pic

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amesema chama hicho tawala kina nguvu na kukubalika lakini kinakwama kwa kusimamisha wagombea wasiokubalika.

Kheri ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 30, 2019 wakati akizungumza na vijana wa umoja huo Mkoa wa Mbeya katika uzinduzi wa kampeni ya Mbeya ya Kijani iliyoambatana na uzinduzi wa daftari la wapiga kura la wanachama wa umoja huo.

Kheri amesema hakuna sababu ya kuingiza mkono iwapo mgombea anayekubalika atapita kwa ridhaa ya wanachama.

“Mtu anayekubarika ndani na nje ya chama lakini akashindwa kwa rushwa au ukabila vijana tunatakiwa kupaza sauti.”

“Tukiruhusu uchaguzi wa mizengwe tutawapa watu kazi ya kuwanadi wagombea wasiokubarika na wananchi,” amesema Kheri.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mashango amesema lengo la mkutano huo ni kutengeneza umoja na mshikamano kwa wanachama pamoja na kuongeza chachu na hamasa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Pia Soma

Katibu wa Hamasa na Chipukizi Mbeya Vijijini,  Kelvin Machango amesema vijana wa umoja huo wanashindwa  kukitetea chama hicho kutokana na hali ngumu ya uchumi licha ya kuwa wanakipenda.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz