Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi akagua zoezi la kupiga kura Mbarali

Mwenyekiti Tume Ya Uchaguzi Akagua Zoezi La Kupiga Kura Mbarali Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi akagua zoezi la kupiga kura Mbarali

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo tarehe 19 Septemba, 2023 ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Jaji Mwambegele baada ya kutembelea vituo amesema ameridhishwa na utendaji wa Wasimamizi wa Uchaguzi huo na kuongeza kwamba vituo vimefunguliwa kwa wakati na zoezi linaendelea vizuri kwa utulivu na amani.

Aidha, Jaji Mwambegele amezungumza na mawakala wa vyama vya siasa ambao wamemueleza kuridhishwa na mwenendo wa zoezi la kupiga kura na kwamba hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza.

Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali unafanyika sambamba na kata sita za Tanzania Bara. Kata zenye uchaguzi ni Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live