Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti Chadema Mbeya akamatwa na polisi

15518 Chadema+pic TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu amekamatwa na Polisi leo alfajiri Jumanne Septemba 4, 2018 akiwa nyumbani kwake.

Baada ya kukamatwa amepelekwa kituo kikuu cha polisi huku sababu za kukamatwa kwake zikiwa hazijulikani.

Akizungumza na MCL Digital mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Mbeya mjini, Elizabeth Mwakimomo amesema taarifa kamili za kukamatwa Mwaipalu wamezipata kutoka kwa mkewe leo asubuhi na tayari viongozi wa chama hicho wameanza kufuatilia.

“Tumekwenda asubuhi kituo kikuu cha polisi tumemkuta lakini tulipomuuliza OCD (Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya) kosa alilofanya amesema hajui kosa,” amesema Elizabeth.

“Tumesubiri hadi mwanasheria wetu, Boniface Mwabukusi afike na alipofika ameamriwa kupelekwa kwa RCO wa Mbeya kwa ajili ya kuhojiwa.”

Alisema viongozi wote wa Chadema mkoa na wilaya za Mbeya wapo kwa RCO wakifuatilia suala hilo na watatoa taarifa kamili za kosa alilokamatiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei alipopigiwa simu kuhusiana na suala hilo, amesema ‘nipo kwenye kikao hapa, naomba nikutafute baada ya muda mfupi. Acha nimalize kwanza hiki kikao ndipo tuzungumze hicho unachotaka kuniuliza.”

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz