Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti CUF wilaya ya Handeni ahamia CCM

Mon, 15 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wilaya ya Handeni mkoani  Tanga, Hassan Hussein amekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichoeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Akizungumza mbele ya viongozi wa wilaya wa CCM wakati akipokelewa katika ofisi ndogo za CCM kata ya Segera wilayani hapa leo, Hassan alisema Rais Magufuli anapambana na mambo yote ambayo upinzani walikuwa wanataka hivyo hakuna sababu ya kuwapo makundi ya kumpinga.

Alisema amechukua uamuzi huo kwa utashi wake mwenyewe bila ya kushawishiwa na mtu kuhama licha ya kwamba huku nyuma kulikua na juhudi hizo ila kwa sasa amekubali kwa hiyari yake.

"Tulikuwa tunapigia kelele rushwa Rais amefanyia kazi, ubadhilifu kwenye miradi na mashirika ya umma pia umepungua sana na mengine mengi mnayaona sasa bora nirudi CCM niwe pamoja na Rais wetu," alisema.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Handeni, Athumani Malunda alisema hakuna mwanachama kutoka upinzani ananunuliwa ila kila mmojakwa sasa anaguswa na CCM mpya ambayo inagusa maslahi ya mwananchi wa chini kabisa kwa kutetea haki za wanyonge kazi inayofanywa na Rais Magufuli.

Alisema sheria na taratibu za vyama zinaruhusu mwanachama kuhamia katika chama anachoona sera zake zinamvutia, hivyo hakuna sababu ya kuwalaumu wapinzani wanaorudi CCM.

Diwani wa Mabanda (CUF) wilayani Handeni, Masoud Mhina amekiri kiongozi huyo alikuwa ni mwenyekiti wake ulikua unakoma Novemba 5 utakapofanyika uchaguzi.

"Huyo mwenyekiti ameona ana hali mbaya kwenye uchaguzi ujao kuwa hatapata tena hiyo nafasi, hivyo ameamua kuhama mapema kabla mambo hayajaharibika ila sisi tunamtakia safari njema" alisema Masoud.

Chanzo: mwananchi.co.tz