Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti CCM Mwanga ashindwa, Hai na Siha wapeta

Images (50).jpeg Mwenyekiti CCM Mwanga ashindwa, Hai na Siha wapeta

Sun, 2 Oct 2022 Chanzo: Mwananchi

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro Jaffar Kandege ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya wajumbe wa mkutano mkuu kumbwaga.

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana Oktoba 1, 2022, Msimamizi wa uchaguzi, Hamisa Chacha amemtangaza Ibrahim Mnzava kuibuka mshindi kwa kupata kura 396.

Amesema katika nafasi hiyo walioshindwa ni Mamboleo Mshana aliyepata kura 166, huku Kandege akipata kura 95.

Katika Wilaya ya Hai, Msimamizi wa Uchaguzi, Zuhura Chikira amemtangaza mshindi wa nafasi ya uenyekiti wa Wilaya kuwa ni Wang’uba Maganda ambapo ametetea nafasi yake kwa kupata kura 335.

Amewataja wengine waliokuwa wakigombea katika nafasi hiyo na kura zao kwenye mabano kuwa ni Ibrahim Ndossa (235) Sophia Viggo (39) na Christopher Madulu (14) ambapo kura zilizopigwa zilikuwa 627, zilizoharibika 4 huku halali zikiwa 623.

Aidha Chikira amewatangaza washindi wa  nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu Taifa, katika Wilaya ya Hai  na kura zao kwenye mabano kuwa ni Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Irando (411) Aikande Raymond Mushi (396) na Rusma Ndosi (388).

Katika Wilaya ya Siha, Msimamizi wa uchaguzi Ramadhan Mahanyu amemtangaza mshindi wa nafasi ya mwenyekiti, kuwa ni Wilfred Mossi ambapo ametetea nafasi yake  kwa kupata kura 429, huku wagombea wenzake Luca Laizer akipata kura 17 na Edina Lukumai akipata kura 10.

Chanzo: Mwananchi